Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]




Hayo Yamezungumzwa na ACP. MJENGI Leo Mei 03,2024  Kwenye kikao na kamati ya usalama wilaya ya Kilombero, Ambapo amesema DKT SAMIA SULUHU HASSAN ametoa Kiasi cha Millioni 800 kwa kuhakikisha mazingira ya jeshi la polisi Wilaya ya  Kilombero yanakuwa safi na salama Ambapo hadi Sasa tayari Milioni 351 zimeshatolewa.

Aidha ACP. MJENGI ameongeza kuwa, Ndani ya miezi minne watahakikisha Ujenzi wa jengo Hilo la kisasa linakamilika Ili lianze kutumika Kwa haraka zaidi. Ambapo kituo iko kipya na cha kisasa kitajengwa katika kata ya Kibaoni tofauti na Pale kilipo kituo kitumikacho kwa sasa.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kilombero Wakili DUNSTAN KYOBYA ambaye ni mwenyekiti wa Ulinzi na usalama katika wilaya hiyo amesema kuwa "Kama kamati wameupokea mradi huo ,huku akimshushukuru RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuwaletea fedha za ujenzi huo na kuwajali wananchi wa Kilombero"

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]