Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]Kocha wa FC Barcelona Xavi Hernández amesema ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu kutokana na matokeo mabaya anayopata na timu hiyo aliyoanza kuinoa Novemba 2021

Ametangaza uamuzi huo baada ya Barcelona kupigika kipigo Cha magoli 5-3 kutoka kwa Villarreal siku ya tarehe 27 January, hivyo kuzidiwa pointi 10 na vinara wa Ligi Kuu ya Uhispania (LaLiga), Real Madrid

Xavi  mwenye umri wa miaka 44, ambaye alishinda mataji 25 akiwa mchezaji wa Barcelona atajiuzulu rasmi Juni 30, 2024 licha ya kuwa amesaliwa na mwaka mmoja zaidi katika mkataba wake na timu hiyo, ameweka wazi kuwa anaamini klabu hiyo inahitaji mbadiliko, akidai kwa sasa wamekuwa wakicheza wakiwa na presha kubwa

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]