Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]


 Kutoka Chuo cha ‘The Recording Academy’ ambacho ni Taasisi na Waandaji wa tuzo kubwa zaidi za muziki duniani za Grammy mapema leo wametoa list ya Wasanii watakaochuana kuwania tuzo mbalimbali za muziki na habari njema ni kwamba staa kutokea nchini Tanzania Rayvanny pamoja na Producer S2kizzy watawania moja ya tuzo hizo kupitia kipengele cha ‘Best Latino Pop Album’ baada ya album ya msanii Maluma aliyewashirikisha wasanii hao wawili kwenye wimbo wa ‘Mama Tetema' kupitia Album yake ya ‘Don Juan’, kuwekwa kwenye list ya album zinazopambania tuzo hiyo.


Wimbo wa ‘Mama Tetema’ ni track namba 21 kwenye album ya Maluma na inawafanya wawili hao kuwa Watanzania wa kwanza kuwania tuzo hizo zitakazofanyika Jumapili, February 4, 2024 kwenye ukumbi wa Crypto.com, Huko Los Angeles nchini Marekani.


Kutoka Africa Msanii Burna Boy amewekwa kwenye vipengele vinne ikiwemo ‘Best Melodic rap Performance', Albamu Bora ya Muziki Ulimwenguni, Utendaji Bora wa Muziki wa Kimataifa na Utendaji Bora wa Muziki wa Afrika Huku Davido akiwa kwenye vipengele vitatu, Asake, Olamide, Ayra Starr na Tyla pia wametajwa kuwania tuzo zao za kwanza za Grammy kupitia ‘Best African Performance’ kilichoanzishwa hivi karibuni kama sehemu ya marekebisho mengi yaliyolenga kufanya mchakato mzima wa tuzo hizo kuwa wenye haki, uwazi na sahihi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]