Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top] Msanii chino kidd amepata ajali akiwa na wenzake safarini kuelekea kwenye show Mkoani Tanga ambapo gari alilokuwa amepanda na baadhi ya Madancer wake (Alphard nyeusi), limegongana na lori la mafuta.


Ajali hiyo imetokea mapema leo maeneo ya Kabuku ambapo Meneja wa Msanii huyo aitwaye Sweder ambaye alikuwa gari la nyuma lililokuwa likiongozana nao amesema “Tulikuwa tunaelekea Tanga katika show ya Mama yetu Ummy Mwalimu, ajali tumeipatia maeneo ya Kabuku, tuliondoka na gari mbili, gari alilokuwa amepanda Msanii lilikuwa imetangulia na Msanii alikuwa amekaa upande wa kushoto wa Dereva”“Gari alilopanda Msanii lilipamiwa na lori la mafuta, tuliweza kupata msaada wa haraka tukafika Hospitali ya Rufaa ya Tanga, alikuja Mama yetu Ummy kutupa support alipofika alituonesha ushirikiano mzuri sana, hakuna aliyefariki, tunamshukuru Mungu, simu ya Msanii ninayo Mimi bado hajapewa ruhusa ya kutumia simu”


“Wote waliopanda kwenye hilo gari wameumia, walioumia zaidi wapo wanne, wengine wanatakiwa kufanya operesheni wameumia zaidi maeneo ya mguu wengine wamevunjika mguu, Dereva amepata mshtuko kwenye kichwa, wengine wamepata shida kwenye taya”

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]