Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]

 


Ilikuwa Agosti 13, mwaka huu Dk Slaa alikamatwa akiwa nyumbani kwake Mbweni na kisha kupelekwa kituo cha Polisi Osterbay, hata hivyo alisafirishwa kwenda jijini Mbeya kabla ya kurejeshwa jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo, na baadaye kuachiwa kwa dhamana.


Akizungumza leo Agosti 18, 2023 muda mfupi baada ya kuachiwa, Dk Slaa amesema hataogopa jela kwani sehemu hiyo imeandalaiwa kwa ajili ya watu, na kwamba ni heri ahukumiwe duniani na mbinguni akapate thawabu kwa kutimiza wajibu wake.


“Bunge tulilolichagua, kama tulilichagua, haliyasemei, lazima sisi wengine tujitose kuyasemea haya ambayo Bunge haliyasemei. Na hili kama litaitwa tena uchochezi, waliite tu, lakini kama Bunge tulilichagua, kuwa wasemaji wetu, na Katiba ibara 62; inawapa mamlaka hayo,” amesema na kuongeza;


Balozi huyo anadhani Bunge halitekelezi majukumu hayo yaliyoainishwa katika ibara tajwa, hivyo amesema: “Wengine tunayaelewa, ambao Mungu alituwezesha tukasoma, Mwenyezi Mungu akatusaidia uwezo wa kujifunza sheria, tutaendelea kuyapigia kelele.”


“Wakituweka ndani tuwekwe tu, si ndiyo maana jela zipo. Unaogopa jela, hatutaogopa jela kwa sababu hata Mungu atatupongeza, atatushukuru, atatutuza, kwa sababu tumetimiza majukumu yetu.”


Akimtolea mfano Askofu Emaus Mwamakula aliyekuwa amekaa pembeni yake, Dk Slaa amesema: “Baba Askofu anajua, kwenye dhamana ya uaskofu wake ana majukumu, asipoyatimiza atahukumiwa, na afadhari uhukumiwe duniani, kuliko hukumu ya Mbinguni, mimi niko tayari nihukumiwe duniani lakini nituzwe mbinguni.”


Amebainisha kuwa hawezi kuacha kushirikiana na Watanzania kujadiliana juu ya rasilimali za nchi na kwa mujibu wa Ibara ya nne ya katiba madaraka aliyonayo Rais anayapata kutoka kwa wananchi.


Amesema mjadaala unaoendelea kwa miezi mitatu kuhusu bandari gati namba moja hadi kumi na mbili tulizojenga wenyewe sijui kama tutashindwa kujenga nyingine.


"Tumekopa fedha nyingi kujenga bandari hata mrejesho fedha tulizokopa kama fefha zimerudi au nani atakayezilipa kama niwananchi au tunaletewa muwekezaji, haya mambo hayatakiwi kuwa ya Siri,"

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]