Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]


 Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu. Mhe.Dkt. Dorothy Gwajima, ameitaka jamii na wanahabari wote nchini, kumuacha Ester Noah, aendelee na maisha mengine badala ya kila wakati kumuweka mitandaoni.


Waziri Gwajima ameyasema hayo, kupitia mitandao yake ya kijamii, ambapo ameendelea kusisitiza kuwa, hata kama Ester amevuka umri wa mtoto, bado ni mtanzania anayehitaji staha na utulivu.


Ikumbukwe Ester Noah, ambaye ni mwananfunzi wa kidato cha tano katika shule ya Sekondari Panda hill iliyopo mkoani Mbeya, alitoweka shuleni mnamo, Mei 18, 2023 katika mazingira ya kutatanisha na alipatikana Juni 23, 2023, katika Mji mdogo wa Mbalizi. 


Aidha Waziri Gwajima amesema kuwa, tayari ametoa maelekezo kwa maafisa ustawi wamfikie Ester, wampe ushauri nasaha kwani ana nafasi ya kuanza ukurasa mpya katika safari yake ya maisha.No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]