Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]

 Ni mara chache sana kuwaona mastaa wote wakubwa duniani kukusanyika sehemu moja, labda liwe Tamasha au mechi ya mpira wa miguu, NBA au SuperBowl, lakini kwenye birthday party huwa mara chache sana hasa kwa mtu ambaye sio msanii au mchezaji.

Bilionea Michael G. Rubin alifanikisha hili siku ya jana baada ya kuwakusanya mastaa wakubwa duniani kwenye sekta tofauti tofauti wakiwemo wasanii wakubwa kama Jay Z, Beyonce, DJ Khaled, Quavo, Frech Montana na wengine lakini pia waigizaji kama Kevn Heart, Kim Kardashian na wengine.

Sio hao tu wachezaji wa mpira wa miguu kama Mbappe na wengine wa mpira w akikapu kama Kevin Durant, sio kitu cha kawaida kuwakusanya wote hao.WENGI WANAJIULIZA HUYU MICHAEL G. RUBIN NI NANI??

Michael G. Rubin huyu ni bilionea anayemiliki kampuni ya kutengeneza na kusambaza nguo za michezo duniani ya Fanatics, Inc. lakini pia alikuwa mmoja wa wamiliki wa timu ya mpira wa kikapu kutoka nchini Marekani ya Philadelphia 76ers mwaka 2011 lakini pia timu ya Hockey ya New Jersey Devils hockey mwaka 2013 kabla ya kuuza hisa zake kwa Harris Blitzer ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya mambo ya kiburudani.

Kubwa zaidi Yeye pia ni mwenyekiti mwenza wa Muungano wa REFORM, shirika la kusimamia haki kwa makosa ya jinai ambalo alizindua Januari 2019, akishirikiana pamoja na Jay-Z, Meek Mill, Robert Kraft, na Daniel S. Loeb.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]