Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]


Madaktari wa idara ya Magonjwa ya Mfumo wa Mkojo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa umebaini kuwa mitindo ya kujamiiana inaweza kusababisha uume uliosimama kwa muda mrefu kuvunjika.

Utafiti wa madaktari hao umechapishwa kwenye Jarida la kimataifa la kesi za Upasuaji (International Journal of Surgery Case Reports, 108(2023)108415) wameripoti kufanya upasuaji wa kuunga uume wa kijana mwenye umri wa miaka 27 uliovunjika wakati akijamiana na mkewe.


Kwa mujibu wa taarifa ya utafiti huo, ajali ya kuvunjika uume si suala lenye kujitokeza mara kwa mara, linauwiano wa 1 kati ya watu 175,000. 


Hata hivyo, utafiti huo unadokeza kuwa, tafiti zilizofanyika katika mataifa ya Ulaya na Marekani zimeonesha kuwa asilimia 93.3 ya ajali za uume hutokana na kujamiiana, ambacho kilikuwa chanzo cha ajali ya Uume aliyopata kijana aliyetibiwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.


Vile vile, ajali za kuvunjika uume kwa kujichua zinashika nafasi ya pili zikiwa na asilimia 10.


Mikao ya kujamiiana kama vile Mwanamke kukalia uume inatajwa kuwa chanzo kikuu cha ajali za kuvunjika uume.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]