Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]

 


Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, Mfaume Mfaume ‘Mapafu ya Mbwa’ amewaomba msamaha mashabiki wake kufuatia kushindwa kuonyesha kiwango kikubwa katika pambano lake dhidi ya Chikondi Makawa wa Malawi, huku akiahidi kujirekebisha kuelekea pambano lake la Septemba, mwaka huu dhidi ya Idd Pialali.


Mwishoni mwa juma lililopita, Mfaume alifanikiwa kuibuka na ushindi wa pointi dhidi ya Chikondi Makawa katika pambano la utangulizi ambapo ni mara ya pili kwa mabondia hao kukutana lakini mashabiki wa Mfaume, hawakuwa wamevutiwa na kiwango alichokionyesha kwenye pambano hilo.


“Nashukuru Mungu kwamba nimeweza kupata matokeo katika pambano lile na Chikondi kwa sababu sikuwa nimejiandaa kwa ajili yake, lakini kutokana na mpinzani wangu kupata changamoto ikanibidi nicheze naye.


“Lakini nataka niwaambie mashabiki wangu, wanisamehe ila ahadi yangu kwao ni kuwa bora katika pambano langu lijalo mwezi wa tisa, naamini nitawapa furaha kubwa kwa mchezo mzuri, alisema Mfaume.No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]