Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]

 


Uongozi wa klabu ya Simba sports club umethibitisha kumsajili mlinzi wa kati Che Fondoh Malone Jr almaarufu ‘Ukuta wa Jericho’ kwa ada ya uhamisho inayotajwa kuwa dola 100,000 (Tsh milioni 243) kutoka klabu ya CottonSports ya Cameroon.


Che Malone (24) raia wa Cameroon amesaini mkataba wa miaka mitatu mpaka Juni 2026 na anatua klabuni hapo kama mbadala wa Joash Onyango (30) aliyetimkia Singida Fontaine Gate FC.


Che Malone ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Ligi Kuu ya Cameroon msimu uliopita wa 2022/23 (2022/23 Cameroon Elite One Footballer of the Year) anatarajiwakwenye tuzo zilizotolewa usiku wa kuamkia leo Jumamosi (Julai 08) na Mboa Foot Awards huko Cameroon.


Che Malone Jr almaarufu ‘Ukuta wa Yericko’ (Wall Of Jericho) Msimu uliopita aliiongoza Cotton Sports kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Cameroon huku akicheza takribani mechi zote kama Nahodha wa klabu hiyo

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]