Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]

 


Pongezi kwa wote ambao mmefanikiwa kuhitimu elimu ya sekondari kwa mwaka huu. Safari inaendelea na huko mbeleni yapo ya kila aina ila wewe unaweza kubaki wa aina hiyohoyo au aina mpya kikubwa ni kwamba maisha hayajasimama. Kama ndivyo basi nawe usisimame au usikubali kwenda na wanaorudi.


Kesho inakungoja, jamii yako inayo mengi yanayoikumba na kuisumbua; inawezekana kabisa kuwa wewe au yule utakayekutana nae kwa sasa ndiye atakusogeza mbali au karibu na hiyo nafasi ya kuleta mabadiliko chanya.


Machache ya kizingatia:-

1. Jipongeze kwa hatua uliyofikia sasa wala usingoje hadi matokeo (matokeo yanakujaga na mengi)


2. Usijipongeze kwa kujihatarisha au kupunguza uwezekano wa kufurahia yajayo (wapo walijikuta wanaanza safari ya malezi eti kisa ni kujipongeza)


3. Kidato cha sita siyo mwisho wala siyo mwanzo bali ni hatua katika safari. Muhimu kuifikia na hatua hiyo ukosogeze karibu na ziliko changamoto za kutatua, fursa za kudaka, n.k


4. Jitahidi kuepuka kuruhusu mtu akuchagulie njia ya kwenda nayo bali sikiliza ushauri, fanya utafiti (inawezekana kuwa na uwezo wa kufanya utafiti mdogo) na kisha chagua njia yako ambayo ukipotea hauna wa kumlaumu na wala hautajilaumu. Kwa mabinti kuwenu makini na kuwaruhu boyfriends wenu kuwachagulia kozi na vyuo vya kusoma.


5. Kwa maisha ya sasa kozi nyingi za kusoma chuo zimebaki majina tu siyo kwamba zina soko kama zinavyodhaniwa. SOKO UNATAKIWA UWE WEWE NA UJUZI WAKO. Jina la chuo pia nalo halina jipya sana ila eneo na mazingira chuo kilipo ndiyo ya Msingi but msingi huo hauna maana sana kama wewe haujatosha.


6. Matokeo ya mtihani yanaweza kukutoa kwenye line ukajikuta ukidondokea ambako utatumia gharama zaidi kujinasua au kudumu huko


7. Safari ya kwenda chuo inaanzaga kwa vifijo, ikihusisha uhuru na mihemko. Esijinyime kufurahi lakini usiishie kwenye kununua simu ya kupiga picha za kupost na nguo nadhifu tu za kwendea kwenye madarasa/ibadani au mitoko ya jioni. Badala yake jiongeze kusogea pale penye kile utakachokiendea wakati unamaliza chuo.


8. Siyo lazima kwenda chuo kikuu mwaka huu au hata badae. Usione aibu kwenda VETA au kwingine wanakofundisha ujuzi unaoweza kutosha kwingi kuliko kwenda kusoma masomo na badae ukaja kujishangaa.


9. Jifunze matumizi yenye tija ya mitandao ya kijamii. Pita route ambayo inaacha tabasamu kwa wenyekukutana na ulichoacha mtandaoni.


10. Tafuta kuelewa na kufahamu hii kitu inaitwa COMMUNICATION SKILLS. Hii ni ya muhimu sana sana. Isivyo bahati vyuoni sina uhakika kama inafundishwa inavyotakiwa. Most importantly hakikisha unafahamu namna ya kuandika Official Email na protocol zake, Sms na WhatsApp Messages, jifunze namna ya kujitambulisha na jinsi ya kushiliki kwenye mazungumzo ya kiofisi au kibiashara


11. Jifunze namna ya kumudu na kutunza muda. Ule muda wa kujiona hauna cha kufanya ndiyo muda sahihi wa kujifunza skills mpya au kujitolea sehemu ambayo utapata uzoefu ambao haupatikani chuoni.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]