Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]


Wala sio tetesi na siri tena

Rasmi Klabu ya Yanga SC wamekamilisha usajili wa kiungo wa soka, Jonas Mkude ' NunguNungu ', 30


 Mkude ambae alikua mchezaji huru baada ya kumaliza miaka zaidi ya 12 akiitumikia Simba SC amesaini mkataba wa miezi 12 kuwatumikia Wananchi


Huu unakua ni usajili wa 03 jumla na wa 02 sasa kwa wachezaji wa ndani kujiunga na mabingwa watetezi wa NBC PL, ASFC, & CS, Yanga SC 


Mkude, ambae ni mkongwe kwa soka la Tanzania lakini pia hata kimataifa, ana ubora mkubwa kwenye eneo la kiungo wa chini lakini pia akiwa na sifa za uongozi akiwa dimbani.


Usajili huu unatokea ikiwa ni siku kadhaa baada ya kukamilishwa kwa usajili wa beki wa pembeni / kushoto ( LB ) Nickson Kibabage, pamoja na beki wa kati ( CB ) Giggy Gift Fred.


Graphic video, iliyotumika kufanya utambulisho wake kidogo inaweza kuibua hisia za tofauti hasa kwa klabu yake ya awali ( Simba SC )


Jonas Mkude, ni Mwananchi na Atakuwepo kwenye mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs, siku ya kilele cha Wananchi

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]