Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]


 Klabu ya Yanga SC imetangaza kukamilisha Usajili wa aliyekuwa Nahodha wa Klabu ya SC Villa ya nchini Uganda na beki wa timu ya Taifa ya Uganda ,Fred Gift Kwa Mkataba wa Miaka Mitatu.


Fred alikuwa miongoni mwa Mabeki watatu waliokuwa wanawania Tuzo ya Beki bora wa Msimu wa Ligi Kuu ya Uganda ambapo Tuzo hiyo ilienda kwa Hilary Mukundane wa Vipers SC ,huku pia akitajwa kwenye kinyang'anyiro cha Tuzo ya Mchezaji bora wa Msimu ambapo tuzo hiyo ilienda kwa Milton Karisa.Licha ya kukosa Tuzo hizo lakini alikuwepo kwenye Wachezaj wanaounda Kikosi bora cha Msimu cha Ligi hiyo.


Kwa Mjibu wa vyanzo vyetu vya karibu na Mchezaji vinadai kuwa alikuwa akitakiwa na vilabu mbalimbali kama Wydad Casablanca,AmaZulu FC na St George ya Ethiopia lakini ofa kutoka Yanga ilimvutia zaidi kabla ya kusajiliwa rasmi.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]