Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]


 Klabu ya Al Ahly imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Misri msimu wa 2022/23, kufuatia kipigo cha mabao 2-1 walichokipata Pyramids FC kutoka kwa Ceramica Cleopatra, usiku huu.


Huo ni ubingwa wa 43 wa Ligi Kuu ya Misri kwa Al Ahly ukiwa ni wa kwanza tangu 2020, baada ya kuwa wameupoteza katika misimu miwili iliyopita Kwa wapinzani wao Zamalek.


Kiujumla huu ni Ubingwa wa tatu kwa klabu hiyo, baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Wydad Casablanca na Ubingwa wa Egypt Super Cup dhidi ya Pyramids FC.


Ahly imetwaa ubingwa huo ikiwa na alama 75 baada ya kucheza michezo 29 ikisaliwa na Michezo mitano, huku Pyramids FC iliyopo nafasi ya pili ikicheza michezo 32 ikiwa na alama 67.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]