Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]


Kampuni binafsi ya Kimarekani "OceanGate" inayoandaa safari za kitalii kwa manowari iliyopotea katika bahari ya Atlantiki imetoa tamko muda mfupi uliopita, ujumbe huo ulisema;

”Hivi sasa tunaamini kuwa Mkurugenzi wetu mkuu Stockton Rush, Shahzada dawood na mtoto wake Suleman Dawood, Hamish Harding na Paul-Henri Nargeolet wamepoteza maisha”

” Mioyo yetu ipo pamoja na roho hizi 5 na wanafamilia wao wote katika wakati huu mgumu sana. Tunaomboleza pamoja nao”

”Familia nzima ya OceanGate inawashukuru sana maafisa wote pamoja na taasisi nyingi zilizoshirikiana nasi kwenye zoezi gumu lililofanyika usiku na mchana kukitafuta chombo”

Mapema leo taarifa kutoka kwa mtaalamu wa uokoaji David Mearns zilieleza kuwa vipande viwili vya manowari iliyokuwa ikitafutwa vilipatikana. Vipande hivyo ni fremu inayotumika wakati wa kutua pamoja na mfuniko wa nyuma wa chombo hiko.

Chombo hicho kilipoteza mawasiliano Jumapili iliyopita wakati kikiwa kwenye moja ya safari zake za kitalii. 


Safari hizo hupeleka watalii chini ya bahari kutizama mabaki ya meli maarufu ya Titanic iliyozama mwaka 1912 katika bahari ya Atlantiki


No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]