Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]


 Kocha Diego Simeone amewatania wachezaji wake nyota wanaofanya mapenzi mara nne kwa mwezi kuwa “Hawawezi kucheza kwenye timu yake”.

Kwenye mahojiano na kituo cha Cadena COPE, Simeone alizungumzia baadhi ya masuala muhimu ya Atletico, ikiwa ni pamoja na kurejea kwa Joao Felix kutoka Chelsea, na mustakabali wake katika klabu hiyo.

Pia ulifika wakati ambao Simeone aliulizwa kuhusu mambo yake binafsi katika mazungumzo hayo ambayo Simeone alishangazwa, baada ya mtangazaji kurejea utafiti unaosema kwamba “Muhispania wa kawaida hufanya mapenzi mara 56 kwa mwaka.

Simeone akajibu: “Mara ngapi? 56... 56 kwa mwaka... Ni mara ngapi kwa mwezi? Nne kwa mwezi? Nne kwa mwezi hapana…

“Mara nne kwa mwezi huwezi kucheza katika timu yangu.”

Kauli hiyo ilipelekea studio za COPE kujawa na vicheko vingi sana.

Waandishi wa kituo hiko walipomshinikiza Simeone kutaja namba yenye uhalisia zaidi, alijibu kuwa “Sitasema namba ... lakini tuna wastani mzuri.”

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 amekuwa akiinoa Atletico Madrid tangu 2011, na tayari amewahakikishia Atletico kushiriki kwenye michuano ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu ikiwa imesalia mechi moja ya kucheza.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]