Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]


Kocha wa Roma Jose Mourinho amepoteza fainali ya shindano la bara Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya Roma kupigwa na Sevilla jijini Budapest

Kocha huyo alikuwa amecheza fainali tano katika mashindano ya Ulaya bila ya kupoteza hata moja lakini sasa hilo limeisha Hili pia ndilo bao la kwanza Jose Mourinho kuruhusu katika fainali za Ulaya tangu mwaka 2003

Roma iliambulia sare ya 1-1 dhidi ya Sevilla ugani Puskas jijini Budapest nchini Hungary lakini wakapoteza 4-1 kwa mikwaju ya penalti na kutia tope rekodi ya Mourinho.

Rekodi ya Jose Mourinho katika fainaliza bara Ulaya

Kocha huyo Mreno alifika katika fainali hii akiwa amecheza fainali tano za mashindano ya bara Ulaya na kushinda zote tano.

Mourinho alishinda kombe lake la kwanza la Ulaya na Porto katika msimu wa 2002/03 - UEFA Cup. Msimu uliofuata akashinda Champions League na klabu iyo hiyo ya Ureno.

Ufanisi wake uliofuata ulikuwa na klabu ya Inter Milan msimu wa 2009/10. Mourinho aliipiga Bayern Munich katika fainali na kushinda kombe la Champions League.

Kocha huyo matata kisha aliiongoza Manchester United kushinda kombe lao la kwanza la Europa katika msimu wa 2016/17 kabla ya msimu jana kushinda makala ya kwanza ya UEFA Conference League na AS Roma.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]