Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]Sehemu ya chini ya maji ina sehemu ya shinikizo ili kuhimili shinikizo la nje chini ya maji. Kwa hivyo, walio ndani wanapaswa kuwa chini ya shinikizo la kawaida la anga kama juu ya ardhi na kupumua hewa ya kawaida.

Hata hivyo, baada ya muda mrefu, oksijeni itatumika na CO2 itazalishwa.

Kulingana na maelezo ya kampuni, manowari hiyo ina uwezo wa kuishi chini ya maji kwa saa 96.

Pia Mtaalamu wa meli ya Titanic Tim Matlin ameambia shirika la habari la Reuters kwamba sakafu ya Bahari ya Atlantiki – eneo ambalo meli ya Titanic - ni "jeusi na lenye baridi kali".

Mbali na hayo, "sehemu ya bahari ni matope na inatiririka. Huwezi kuona mkono wako mbele ya uso wako. Njia pekee ya kupata mahali ulipo ni kwa kitu kinachoitwa sonar. Hata rada haifanyi kazi," alisema.

Matlin aliongeza: "Kwa hiyo ninahofia maisha ya watalii hao ambao wako kwenye meli."

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]