Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]

 


FUNGA YA SIKU YA ARAFA


Inafahamika vizuri kuwa siku ya arafa ni siku ya tisa ya mwezi wa hija (mfunguo tatu), kwa hiyo mwenye kutaka fadhila za funga ya siku ya arafa anatakiwa afunge siku ya tisa na mwezi wa hija (mfunguo tatu), ndio wakati wake, na kwa sababu Allah amejaalia majira kutafautiana baina ya miji ya mbali ndio kukawa kuna tafauti pia ya nyakati za usiku na mchana, kuchomoza jua na mwezi na kutua kwake, na kuandama kwa mwezi baina ya miji ya mbali sana.


Na kwa sababu hiyo Muislamu anatakiwa afunge siku ya arafa ambayo ni siku ya tisa ya mwezi wa hija (mfunguo tatu) kwa mujibu wa muandamo wa mji aliopo au miji ya nchi aliyopo, na si kwa muandamo wa Makka wala mji wowote mwengine isipokua kama anaishi katika mji wa Makka au mji husika.


Hivo ndivyo ilivyofanyiwa kazi makarne yote yaliyopita wala haijulikani khilafu.

Kwa hiyo msimamo wa kufuata muandamo wa Makkah tu ni Bidaa Potofu tujihadhari nayo.


No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]