Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]

 


Watu watano akiwemo Mtoto wa kike mwenye umri unaokadiriwa kuwa miaka nane hadi tisa wamethibitika kufariki dunia huku Watu kadhaa wakijeruhiwa katika ajali ya basi la New Force lenye namba za usajili T173 DZU linalofanya safari zake Dar es salaam - Rukwa baada ya basi hilo kuanguka wakati liki-overtake lori darajani na kupoteza uelekeo kisha kugonga daraja na kuingia mtaroni katika kijiji cha Igando Kata ya Luduga Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani wa Njombe.

Akiongea kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, John Makuri Imori, amesema hizo ni taarifa za awali lakini atatoa taarifa zaidi baadaye.

"Kwa taarifa za awali basi la New Force lilikuwa linatoka Dar es salaam kwenda Rukwa, lilipofika Igando kuna sehemu ya daraja likawa linataka kuovartake likapoteza uelekeo likagonga daraja likaingia mtaroni, tupo eneo la tukio kwa sasa hatujajua majeruhi ni wangapi lakini zenye uhakika hapa ni maiti nne wakiwemo Wanaume wanne na Mtoto mmoja”

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]