Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]


Kaandika Haji manara kwenye ukurasa wake wa Instagram Ujumbe mzito kwa mama Samia


"Kwako Rais wangu Mpendwa Mh Mama @samia_suluhu_hassan

Chochote nitakachoandika kwako hakikidhi neno la Shukran Kwa hili unalotufanyia Watu wa Sports hususan football, unatupa nguvu ya ajabu ww na Serikali yako, unatupa heshma kubwa na unaonyesha dhamira ya dhati ya kuupeleka mbele zaidi mchezo huu unaopendwa zaidi nchini na kote Ulimwenguni.

Unakuwa Rais wa kwanza wa Tanzania kutoa Ndege kuisafirisha Team ya Mpira kusafiri umbali mrefu kwenda kupigania Nchi,hajafanya yoyote kabla yako, na sio ndege tu, ni Dreamliners, Dege kubwa lenye Engen za kutosha kusafiri umbali wa masafa ya kutosha

Umeshiriki direct kuwapa hamasa Wachezaji wetu wa Team mbili Wawakilishi wa Taifa, ili tu kuwatia nguvu ya kushinda Kwa kuahidi Pesa ambazo ,ungeweza kabisa kuzielekeza zikatatue changamoto nyingine za jamii yetu unayoiongoza ww Mama yetu mpendwa.

Mara kadhaa umetoa neno kuhusu Sisi Watu wa Soka, aidha Kwa kutuasa, kutupongeza na hata kututia moyo, umekuwa chachu kubwa ya mafanikio ya Yanga Msimu huu kwenye mashindano ya kimataifa, imagine yale maamuzi yako ya kuunga mkono uenyeji wa Mashindano ya AFCON 2027 yanakuweka wapi katika mioyo ya Wanazi wa kandanda nchini!!

Umaarufu ulionao kwetu sio wa uoga bali ni wa mapenzi makubwa unayotupa jamii ya Wanamichezo kote Tanzania, huku Site wewe ni Mashuhuri kweli kweli, Watu wanakuzungumza very positive na mahaba ya Wananchi wako sio ya kuigiza hata kidogo.

Mama, Football ni mchezo unaopendwa mno na Watu wako na unavyoendelea kutuunga mkono kwa ukubwa huu, unatengeneza kitu kikubwa sana ktk nyoyo zetu, wenyewe Watu wa Soka tunasema unajipigia Pasi ya mbele ili uje kufunga kirahisi muda ukifika, unamwaga Majalo kama Lomalisa kisha unakuja kufunga kama Mayele.

Once again Tunasema Asante,

Kiufupi unaongoza nyoyo zetu na sio Viwiliwili vyetu, Tuliopo huku Mtaani na mitandaoni tunajua jinsi ulivyotushika Watanzania, Ngoma ikiitishwa leo, Jua halizami ,utakuwa ushachukua ushaweka WAAAAA

Kila la kheri kwako Madame President wa Nchi, Mungu akuhifadi na kila balaa na hasadi, akulinde na uadui wa Siri na wa hadharani, aendelee kukupa Tawfiq na Nishati ya kutuongoza, Akuzidishie Imani na Subira na akupe mwisho mwema Amiri wetu mkuu 🙏🙏"

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]