Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]

Tottenham wamedhamiria kuzima majaribio ya Manchester United ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa England Harry Kane, 29, msimu huu wa joto, huku mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy akigoma kumuuza Kane kwa timu pinzani ya Ligi kuu England. chanzo Cha habari (Mirror)

Kocha wa Manchester united Erik ten Hag ana imani kuwa anaweza kumshawishi kiungo wa kati wa Chelsea Mason Mount mwenye umri wa miaka 24 ajiunge na Manchester United kama sehemu ya maboresho ya kikosi chake kwenye usajili wa majira ya joto. chanzo Cha habari (Telegraph)

Klabu ya ujerumani Bayern Munich wako tayari kulipa pauni milioni 95 kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, huku timu hiyo ya Ujerumani ikiwa na nia ya kuipiku Arsenal katika kuinasa saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. chanzo Cha habari ni (Mirror)

Pia Crystal Palace wamemtafuta mkufunzi wa zamani wa Chelsea na Brighton Graham Potter kuziba nafasi ya kocha iliyo wazi, huku Nice pia ikimtaka Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 48.

Liverpool wamekataa ofa ya kudumu ya uhamisho kutoka nje ya nchi kwa kiungo mshambuliaji wa Ureno chini ya umri wa miaka 21 Fabio Carvalho huku klabu hiyo ya Merseyside ikifikiria kumtoa kwa mkopo tu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20.

Kocha wa Barcelona Xavi amekiri kuwa yuko kwenye mazungumzo na mshambuliaji wa Argentina na Paris St-Germain Lionel Messi mwenye umri wa miaka 35 kuhusu kurejea Camp Nou msimu wa joto. (Standard)

Chelsea wameanzisha mazungumzo kuhusu mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Uruguay na Sporting CP Manuel Ugarte, 22. (90Min)

Crystal Palace wanafikiria kumchukua kwa mkopo kiungo wa kati wa Chelsea na England wa chini ya umri wa miaka 19 Lewis Hall, 18. (Mail)

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]