Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]


Ili kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa katika klabu ya Simba msimu ujao, mabosi wa Simba wameamua kumzuia beki wa kushoto na nahodha msaidizi wa kikosi hicho, Mohamed Hussein 'Tshabalala' kwa kumwekewa Sh300 Milioni mezani ili asiende klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini iliyokuwa inammnyemelea ili imsajili

Tshabalala amebakiza mechi mbili tu kuuaga msimu huu na kumaliza mkataba alionao kwa sasa, lakini ni mmoja wa mabeki ambao Kocha Roberto Oliveira 'Robertinho' anayetaka kuona anasalia kikosini na fasta mabosi wa klabu hio wameamua kumpa mkataba mpya wenye dau nono.

Nahodha huyo msaidizi aliwapa kazi ngumu mabosi wa timu hiyo kumbakiza Msimbazi kutokana na ofa kubwa aliyokuwa amepewa na Kaizer Chiefs iliyowekwa dau la Sh400 Milioni na mshahara wa Sh30 Milioni kwa mwezi, lakini walipambana na kumalizana naye na beki huyo kusaini dili jipya.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]