Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]


Recep Tayyip Erdogan ameibuka na kuwa gwiji wa kisiasa ambaye ameiongoza Uturuki kwa miaka 20 na ameweka alama yake nchini humo pengine kuliko kiongozi yeyote tangu Mustafa Kemal Ataturk, baba wa taifa na rais wa kwanza wa taifa hilo.

Jumapili ya tarehe 28 mei,2023. alifanikiwa kurejesha mamlaka yake kwa miaka mitano zaidi kwa kumshinda mgombea wa upinzani Kemal Kilicdaroglu katika duru ya pili ya uchaguzi uliokuwa na ushindani wa karibu ambao mtawala huyo amelazimika kugombea katika miongo miwili.

Katika asilimia 99.85% ya kura zilizohesabiwa, Erdogan alipata asilimia 52.16% ya kura huku mgombea wa upinzani akipata asilimia 47.84%, kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka za Uchaguzi za Uturuki.

Saa chache kabla ya matokeo rasmi kutangazwa, Erdogan alikuwa amejitangazia mshindi, huku mpinzani wake - bila kukubali ushindi - alielezea mchakato huo kuwa "usio wa haki".

Kilicdaroglu, ambaye aliweza kuunganisha vyama vyote vya upinzani nchini humo, na kutoa upinzani mkubwa zaidi dhidi ya Erdogan tangu aingie madarakani mwaka 2003.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]