Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]


Leo hii spika wa Bunge la Uganda Anita Among ametangaza kuwa Rais Museveni ameutia saini muswada wa kupinga mapenzi ya jinsia moja kuwa sheria.

Spika Anita Among , amesema Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, ametekeleza majukumu yake ya kikatiba kama ilivyoainishwa na Ibara ya 91 (3) (a) ya Katiba. Ameidhinisha Sheria ya Kupinga mapenzi ya jinsia moja, aliandika katika taarifa yake aliyoituma kwenye mtandao wa Twitter.

''Kama Bunge la Uganda, tumejibu kilio cha wananchi wetu. Tumetunga sheria ili kulinda utakatifu wa familia kulingana na Kifungu cha 31 cha Katiba ya Uganda''.

Lakini mswada wa Kupinga mapenzi ya jinsia moja unalenga kwenda mbali zaidi na kuwafanya watu kuwa wahalifu kwa msingi wa utambulisho wao wa kijinsia.

Mtu anayepatikana na hatia ya kulea au kusafirisha watoto kwa madhumuni ya kuwashirikisha katika vitendo vya wapenzi wa jinsia moja anakabiliwa na kifungo cha maisha jela.

Watu binafsi au taasisi zinazounga mkono au kufadhili shughuli au mashirika ya haki za LGBT, au kuchapisha, kutangaza na kusambaza nyenzo na fasihi za vyombo vya habari vinavyounga mkono wapenzi wa jinsia moja, pia watakabiliwa na mashtaka na kufungwa gerezani.

Chini ya sheria iliyopendekezwa, marafiki, familia na wanajamii watakuwa na wajibu wa kuripoti watu walio katika mahusiano ya jinsia moja kwa mamlaka.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]