Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]


Leo siku ya mei 31 taarifa zinasema kuwa Pande zinazozozana nchini Sudan zimekubali kuongeza muda wa usitishaji mapigano kwa siku tano zaidi, baada ya upatanishi uliofanywa na Marekani pamoja na Saudi Arabia.

Hata hivyo Nchi hizo mbili kwa pamoja zilisema kwamba ingawa usitishaji wa mapigano haujazingatiwa kikamilifu uliruhusu kupelekwa kwa misaada katika maeneo ya Sudan.

Ingawa jeshi la Sudan na hasimu wake, kikosi cha msaada wa maraka (RSF), wameahidi kusitisha mashambulizi ya anga, mizinga na mapigano ya mitaani, hakuna upande unaozingatia kikamilifu ahadi hiyo ya kusitisha mapigano.

Hakuna njia za kibinadamu ambazo zimetengwa hadi sasa kusaidia kuingiza misaada na kuokoa watu, huku misaada ikifika katika maeneo machache ndani ya mji mkuu Khartoum.

Kuongezwa kwa siku tano kwa mapatano hayo kutatoa muda wa kusaidia watu kwa misaada ya kibidamu, kurejesha huduma muhimu, na majadiliano ya uwezekano wa kusitishwa kwa mapigano kwa muda mrefu.

Mapambano makali ya madaraka yaliyoanza katikati ya mwezi wa Aprili yameugeuza mji wa Khartoum na maeneo mengine ya mijini kuwa uwanja wa vita na hospitali kuwa vituo vya kijeshi.

Mamia ya watu wameuawa na karibu watu milioni 1.4 wamelazimika kuyakimbia makazi yao.


No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]