Drone Online

KARIBU YAKO KWA HABARI ZA UHAKIKA,MAKALA,MICHEZO,MITINDO YA MAISHA NA BURUDANI

Post Page Advertisement [Top]


Baada ya kumaliza katika nafasi ya 12 katika msimu wa 2022/23 katika ligi ya uingereza klabu ya Chelsea imemtangaza Mauricio Pochettino (51) kuwa Kocha wao Mkuu mpya kwa mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.

Pochettino ataanza rasmi kazi ya kuifundisha Chelsea kuanzia July 1 2023 ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu England 2023/2024.

Kabla ya kujiunga na Chelsea, Pochettino ambaye ni Raia wa Argentina amewahi kuvifundisha vilabu vya Espanyol (2009-2012), Southampton (2013-2014) Tottenham (2014-2019) na PSG (2021-2022)

Huenda mwakani klabu ya Chelsea inaweza kulud katika nafac zake Bora za juu kama walivyozoea mashabiki wa klabu hiyo

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]